Mkurugenzi Wa Urasimishaji Wa Rasilimali Na Biashara at Mkurabita
- Company: Mkurabita
- Location: Tanzania
- State: Dar Es Salaam Jobs
- Job type: Full-Time
- Job category: Graduates Jobs in Tanzania
Job Description
Mkurabita
POST MKURUGENZI WA URASIMISHAJI WA RASILIMALI NA BIASHARA – 1 POST
POST CATEGORY(S) BANKING, ECONOMICS AND FINANCIAL SERVICES
HR & ADMINISTRATION
LAND MANAGEMENT
MARKETING,MEDIA AND BRAND
EMPLOYER Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge – Mkurabita
APPLICATION TIMELINE: 2020-08-25 2020-09-08
JOB SUMMARY NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
i.Kuandaa na kufanya Mapitio ya Miongozo ya urasimishaji wa rasilimali na biashara kwa ajili ya kutekeleza shughuli za urasimishaji Tanzania.
ii.Kuandaa na kufanya mapitio ya vigezo vinavyotumika kuchagua maeneo ya utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali na biashara kila mwaka kwa Tanzania.
iii.Kusimamia utekelezaji wa urasimishaji wa biashara kwa Mfumo wa kuanzisha Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara katika Malmalaka za Serikali za Mitaa za Tanzania.
iv.Kusimamia utekelezaji wa urasimishaji rasilimali ardhi Mijini na Vijijini Tanzania.
v.Kubuni, Kuandaa na Kutekeleza Programu za kuwajengea uwezo wananchi waliorasimisha rasilimali ardhi na biashara zao ili kuzitumia katika kupata mitaji kutoka Taasisi za fedha kwa ajili ya shughuli za kiuchumi
vi.Kuandaa na kutekeleza Mpango na Bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa rasilimali na biashara Tanzania.
vii.Kubainisha na kutoa ushauri wa utatuzi wa changamoto ambazo zinabainika wakati wa utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali ardhi na biashara Tanzania;
viii.Kushirikiana na Mtaalam wa Utafiti, Ufuatiliaji na Tathmini kufanya Utafiti, Ufuatiliaji na Tathimini ya utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa rasilimali na biashara Tanzania. Aidha, Mkurugenzi wa Urasimishaji, anao wajibu wa kufanya tafsiri ya matokeo ya utafiti, fuatiliaji na tathmini na kuandaa mpango kazi wa utekelzaji wa mapendekezo yanayotolewa;
ix.Kushirikiana na Mtaalamu wa Mawasiliano kwa Umma katika kuhamasisha na kujenga hamasa kwa wamiliki wa rasilimali na biashara ili waweze kurasimisha na kuzitumia rasilimali ardhi na biashara zao kwa shughuli za kiuchumi;
x.Kusimamia na kuratibu uaandaji wa taarifa ya utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali na biashara katika vipindi vya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka Tanzania;
xi.Kubuni na kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayolenga kuboresha mchango wa ajenda ya urasimishaji katika kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja;
xii.Kubuni na kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayolenga kuchochea uendelevu wa matokeo ya urasimishaji wa rasilimali na biashara nchini.
xiii.Kazi zingine ambazo atapangiwa na Mratibu wa Mpango;
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
i.Awe na Elimu ya kiwango cha shahada ya Uzamili katika moja ya maeneo yafuatayo:- Uchumi, Uongozi wa Biashara, Ujasiriamali na Usimamizi wa Ardhi.
ii.Awe na Uzoefu usiopungua miaka mitano (5) katika kubuni, kuandaa na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwa wananchi wanyonge wa Tanzania.
iii.Awe na uzalendo na uadilifu usio na mashaka na awe tayari kutekeleza majukumu yake bila usimamizi na mwenye kujituma mwenyewe na awe na uwezo wa kuongoza na kusimamia wengine.
iv.Awe na uwezo wa kuwasiliana katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza
v.Awe na ujuzi wa komputa kutumia “Microsoft Word, Microsoft Excel na Power point”
vi.Awe na umri usiozidi miaka 55.
REMUNERATION Ngazi za Mishahara za MKURABITA
Method of Application
Submit your CV and Application on Company Website : Click Here
Closing Date : 26th September, 2020.
Dont Miss Latest Jobs In Tanzania. Subscribe Today. CLICK HERE